Harmonize adai heshima kutoka kwa Wakenya

Muhtasari

•Staa huyo wa Bongo amedai kwamba alifanya vyema zaidi katika kifungo chake cha wimbo wake na Otile Brown ambao hujaachiliwa bado.

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Tanzania Rajab Abdul Kahali almaarufu kama Harmonize ametoa ombi kwa Wakenya kumpa heshima zaidi kufuatia collabo yake mpya na Otile Brown.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa Bongo amedai kwamba alifanya vyema zaidi katika kifungo chake cha wimbo huo ambao bado haujaachiliwa.

Kutokana na hayo Harmonize ameomba mashabiki wa muziki haswa kutoka Kenya kumpa  heshima zaidi.

"Tafadhalini kila mtu haswa Wakenya, mnipe heshima kwa jinsi nilivyoua katika wimbo wa @otilebrown" Harmonize aliandika.

Gwiji wa muziki nchini Kenya Otile Brown amekubaliana na kauli ya Harmonize huku akihakikishia mashabiki kwamba kweli kifungo chake ni cha kusisimua.

Otile amesema kwa sasa anashughulika na mazishi ya nyanyake yatakayofanyika wikendi ijayo kisha baadae kibao alichofanya na Harmonize kiachiliwe.

"Kweli, aliua katika kifungo chake. Nyote mnajua Obizee huwa haangushi. Tunazika nyanya wikendi hii kisha tutawale" Otile amesema.

Otile Brown alitangaza kifo cha nyanya yake wiki iliyopita.