Umenikosea heshima sana, Presenter Ali amkashifu Magix Enga

Muhtasari

• Mwanablogu, Presenter Ali amemkashifu vikali msanii Magix Enga kwa kile anachokitaja kuwa ni kutumia jukwaa lake kutoa stori za uongo ili kufufua kipaji chake ambacho kilikuwa kimeonekana kufifia.

• Presenter Ali ambaye ameonekana kuwa mwenye gadhabu katika video moja aliyoiachia katika mtandao wa YouTube akisema kwamba, msanii huyo ambaye pia ni mzalishaji wa muziki amemkosea heshima na kusisitiza kuwa hakuhusika kivyovyote vile katika njama hizo za Magix Enga kuwahadaa mashabiki.

• Presenter Ali amewaomba msamaha mashabiki wake na kuahidi kuzidi kuwapa kazi za kuburudisha.

Presenter Ali
Presenter Ali
Image: Instagram KWA HISANI

Mwanablogu, Presenter Ali amemkashifu vikali msanii Magix Enga kwa kile anachokitaja kuwa ni kutumia jukwaa lake kutoa stori za uongo ili kufufua kipaji chake ambacho kilikuwa kimeonekana kufifia.

Presenter Ali ambaye ameonekana kuwa mwenye gadhabu katika video moja aliyoiachia katika mtandao wa YouTube akisema kwamba, msanii huyo ambaye pia ni mzalishaji wa muziki amemkosea heshima na kusisitiza kuwa hakuhusika kivyovyote vile katika njama hizo za Magix Enga kuwahadaa mashabiki.

“When I reached out to Magix Enga sikujua tunaenda kuzungumzia nini. Nikaingia kwenye set nikamuuliza one question amepotelea wapi, and the next thing he said was he has seen people on my channel talk about Illuminati and that thing is real and he went ahead na kuzungumzia experience yake,” alisema presenter Ali.

Image: MAGIX ENGA

Ali ambaye pia alikuwa mtangazaji katika kituo kimoja cha televisheni humu nchini amesema kuwa, kubuni vipindi vya YouTube inamtengenezea maisha kama kazi yoyote ile na hivyo basi watu wanapaswa kuwaheshimu ‘content creators’ na sio kuwatumia kutafuta umaarufu.

Kulingana na Presenter Ali ni kwamba Magix Enga amefaidika na watu elfu kumi [10,000] zaidi ambao wamefuatilia akaunti yake ya YouTube tangu afanye mahojiano hayo, na itakuwa jambo la kukera iwapo atakuwa anawafanyia shere mashabiki hao ambao walikuwa wamekwenda pale kumsaidia kusukuma muziki wake.Aidha ametishia kwamba atawaambia ‘content creators’ wengine wasijihusishe naye na kutowafanyia ,mahojiano wasanii wengine wenye tabia sawia na zake.

Presenter Ali amewaomba msamaha mashabiki wake na kuahidi kuzidi kuwapa kazi za kuburudisha.