Michelle Ntalami afunguka kuhusu maisha baada ya kutengana na Makena Njeri mwaka jana.

Muhtasari

• Mwanabiashara Michelle Ntalami amesema kwamba ilimchukua muda mrefu kusahau kilichotokea  baada ya mahusiano yake na Makena Njeri kusambaratika mwaka wa 2021.

• Akizungumza kwenye mahojiano na Dr. Ofweneke Jumatatu 31/01/2022 , Ntalami ameweka wazi kwamba alifanya kila kitu kutunza penzi lao ila Makena akakosa kuwa mwaminifu na kuheshimu uhusiano wao.

Michelle Ntalami
Image: Hisani

Mwanabiashara Michelle Ntalami amesema kwamba ilimchukua muda mrefu kusahau kilichotokea  baada ya mahusiano yake na Makena Njeri kusambaratika mwaka wa 2021.

Akizungumza kwenye mahojiano na Dr. Ofweneke Jumatatu 31/01/2022 , Ntalami ameweka wazi kwamba alifanya kila kitu kutunza penzi lao ila Makena akakosa kuwa mwaminifu na kuheshimu uhusiano wao.

Ntalami alisema kwamba kitendo hicho kilimpelekea kujichukia na hata kukata mawasiliano baina yake na Makena Njeri ili kusonga mbele kimaisha.

Aidha mwanabiashara huyo ambaye ameonekana kuzungumza wazi kuhusu yeye kushabikia mapenzi ya jinsia moja, amekiri kwamba licha ya yeye kuwa na roho nzuri ya kutangamana na watu, ishu hiyo ilimsababisha kukata tama na kuumia kwa kiasi kikubwa.

Ameongezea kuwa alimpa Makena Njeri nafasi ya kueleza kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea ila mpenziwe akaamua kupotezea swala hilo, ila baadaye ukweli ukajitokeza na hilo ndilo lililomuumiza sana.

Akizungumza kwa hisia nyingi, Ntalami alikiri kwamba kutengana na Makena Njeri kulisambartisha biashara yake na hata kupoteza mamilioni ya fedha, ila amewaahidi mashabiki wake kwamba amejipanga vilivyo na atafanya kila kitu kutimiza haja za wanunuzi wake.

Hata hivyo, Ntalami amekiri kwamba, kwa sasa hali yake ni nzuri na maisha yake yameanza kurejea kawaida. Amesisitiza kwamba kilichomsaidia ni yeye kuzunguza na rafiki zake kuhusu akichokuwa anakipitia wakati huo.

Kwa sasa Ntalami anajikita zaid katika biashara zake na kufanya mambo yanayofurahisha roho yake.