Ronaldo aweka rekodi ya wafuasi milioni 400 Instagram

Muhtasari

• Mchezaji wa soka maarufu kote duniani Mreno Christiano Ronaldo ameandikisha rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kufikisha wafuasi milioni 400 katika mtandao wa Instagram.

• Mreno huyo ameandikisha rekodi hii ambayo haijawahi kutokea tangu uzinduzi wa mtandao huo wa Instagram, siku moja tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufikisha miaka 3

Ronaldo na Mkewe katika hafla ya siku yake ya kuzaliwa
Image: Christiano Ronaldo (Facebook)

Mchezaji wa soka maarufu kote duniani Mreno Christiano Ronaldo ameandikisha rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kufikisha wafuasi milioni 400 katika mtandao wa Instagram.

Hii si mara ya kwanza kwa mwanasoka huyo kuvunja na kuandikisha rekodi mpya kwani imekuwa ni kama mazoea kwake.

Ikumbukwe mwaka jana Ronaldo aliandikisha rekodi kwenye Guinness Book of Records kwa kuwa mchezaji mwenye mabao mengi Zaidi (110) katika mechi za kitaifa, akipiku rekodi ya mchezaji wa Iran, Ali Daei ya mabao 109, rekodi ambayo  ilikuwa imesimama kwa muda mrefu Zaidi.

Mreno huyo ameandikisha rekodi hii ambayo haijawahi kutokea tangu uzinduzi wa mtandao huo wa Instagram, siku moja tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufikisha miaka 37, katika sherehe ya kibinafsi ambayo walisherehekea na mkewe.

Image: Instagram (Screenshot)

Mchezaji huyo nguli anayekipiga na klabu ya Manchester United alisherehekea siku yake ya kuzaliwa siku moja baada ya kubanduliwa nje ya dimba la FA na malimbukeni Middlesbrough, mechi ambayo Ronaldo alipoteza penati.

Mashabiki wa mchezaji huo kote duniani wamempa hongera kwa rekodi hiyo ya Instagram.

Ama kweli Mungu akiamua kumpa mja wake, humpa hadi na nyongeza!