Simchukii Rotimi ila sisikizi nyimbo zake -Juma Jux

Muhtasari

• Msanii kutoka taifa la Tanzania, Juma Jux amekiri kwamba huwa hasikilizi nyimbo za muimbaji Rotimi.

• Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari huko Bongo, Jux amesema kwamba yeye anapenda kusikiliza nyimbo za wasanii wa kitambo na hivyo basi hilo halitoi ruhusa kwake yeye kusikiliza ngoma za Rotimi ambaye ni msanii wa kizazi cha kisasa.

Msanii kutoka taifa la Tanzania, Juma Jux amekiri kwamba huwa hasikilizi nyimbo za muimbaji Rotimi.

Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari huko Bongo, Jux amesema kwamba yeye anapenda kusikiliza nyimbo za wasanii wa kitambo na hivyo basi hilo halitoi ruhusa kwake yeye kusikiliza ngoma za Rotimi ambaye ni msanii wa kizazi cha kisasa.

“Unajua mimi kusikiliza kwanza nyimbo, yaani mimi nyimbo ambazo nazisikiliza ni za zamani sana, yaani wasanii wapya wapya sisikilizi sanaa so nisiongee uongo,” alisema Jux.

Ifahamike kwamba Rotimi ndiye mume wa Vanessa Mdee ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wake Juma Jux huku wengi wakidadisi kwamba Jux alitoa kauli hiyo kwa sababu ya machungu aliyo nayo kwake kwa ‘kumuibia’mpenzi.

Jux ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana kuachia picha kwenye mitandao akiwa na anayekisiwa kuwa mpenzi wake mpya, anaaminika kuamua kusonga mbele baada ya mahusiano yake ya awali kusambaratika nay yeye kuwa bila mpenzi kwa muda mrefu.