EP ya Otile Brown kudondoka tarehe 10/2/2022

Muhtasari

• Msanii Otile Brown ametangaza kwamba atakuwa anaachilia EP yake ya kwanza mwaka wa 2022 siku ya Alhamisi .

• Ngoma  zote tano kwenye EP hiyo ya #UptownFlex zitakuwa na ‘title’’ za kizungu licha ya wengi kumfahamu Otile Brown kupitia umahiri wake katika nyimbo za Kiswahili.

Msanii Otile Brown ametangaza kwamba atakuwa anaachilia EP yake ya kwanza mwaka wa 2022 siku ya Alhamisi .

Otile ambaye siku ya Jumanne alionekana akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji, amewaomba mashabiki kusapoti EP hiyo ambayo itakuwa na ngoma tano kwa ujumla.

Ngoma  zote tano kwenye EP hiyo ya #UptownFlex zitakuwa na ‘title’’ za kizungu licha ya wengi kumfahamu Otile Brown kupitia umahiri wake katika nyimbo za Kiswahili.

Hatua hii inajiri wiki kadhaa baada yake kuachia kibao kikali na msanii kutoka Tanzania, Harmonize ambacho kilionekana kupendwa na mashabiki wengi, na hata kutinga ‘views’ zaidi ya milioni mbili katika mtandao wa YouTube.

Ukwasi na ukali wa staa huyu kwenye muziki umeweza kudhihirika kwa muda mrefu sasa huku wengi wakisubiri kusikia utofauti katika EP hiyo.