Urafiki wa Dorea na Mylee bado upo licha ya wote kunasa kwa Weezdom

Muhtasari

• Mylee Stacey amefichua kwamba bado urafiki wake na muigizaji Dorea Chege almaarufu Maggie bado upo licha wote kuwa na mahusiano na Weezdom

• Stacey ambaye mahusiano yake na msanii Weezdom yamekuwa yakisuasua amesema kwamba katu hana chuki na Chege kwa kitendo hicho cha kumchukulia mume wake

Dorea Chege na Mylee Stacey
Image: INSTAGRAM

Mylee Stacey ambaye wiki moja iliyopita alitangaza kujitosa katika siasa kuwania ubunge wa Kibwezi Magharibi amefichua kwamba bado urafiki wake na muigizaji Dorea Chege almaarufu Maggie bado upo kwa sana licha ya wawili hao kuwahi kuwa katika mahusiano na mwanaume mmoja ambaye ni msanii wa injili, Weezdom.

Stacey ambaye mahusiano yake na msanii Weezdom yamekuwa yakisuasua amesema kwamba katu hana chuki na Chege kwa kitendo hicho cha kutoka kimapenzi na mumewe Weezdom.

Amesema yeye bado ni Rafiki wa karibu sana na Chege ambaye pia alitangaza kuwania uwakilishi wa kike katika kaunti ya Nairobi.

Akihojiwa na mtangazaji Mwende Macharia, Mylee alisema urafiki wao na Chege bado upo hata ingawa hawazungumzi sana kama ilivyokuwa hapo awali.

“Hatuna uadui. Sisi wote tunashughulika sana katika kampeni,” alisema Mylee.

Alipoulizwa ni kwa jinsi gani anavyopelekana na wapenzi wa msanii Weezdom, Stacey alisema kwamba hawana uhusiano wowote na wazazi wenza Weezdom kwa sababu kila mmoja ana Maisha yake na hajawahi kumshrutisha jinsi ya kuwashughulikia watoto wake hata mara moja.

“Ningependa kumtaka ashughulikie watoto wako, na katika hilo sina tatizo

Katika siku za hivi karibuni, Stacey amefichua kwamba alionywa dhidi ya kuingia katika mahusiano na msanii Weezdom ila hakusikia.

Stacey analenga kiti cha ubunge Kibwezi Magharibi kupitia mwavuli wa Azimio la Umoja, huku akitarajia kupata tiketi ya chama cha ODM.