Ahsante kwa kunichagua mimi! Brown Mauzo amwambia Vera Sidika

Muhtasari

• Msanii wa mitindo mipya Brown Mauzo alimsherehekea mpenzi wake Vera Sidika kwa ujumbe maalum siku ya Valentino, Februari 14.

• Ahsante kwa kunichagua mimi,” Brown Mauzo aliandika kwenye Instagram

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Msanii wa mitindo mipya Brown Mauzo alimsherehekea mpenzi wake Vera Sidika kwa ujumbe maalum siku ya Valentino, Februari 14.

Kwenye Instagram yake, Brown Mauzo amemsherehekea Vera Sidika na kumshukuru kwa kumchagua yeye kuwa mumewe na baba wa mtoto Asia, kwani hiyo ni bahati adimu sana kama kuuona mkojo wa kuku ashakum si matusi.

“Najitolea hii siku nzuri na kumpa mazima mpenzi wangu wa Maisha @queenveebosset. Ahsante kwa kunichagua mimi,” Brown Mauzo aliandika kwenye Instagram

Msanii huyo pia amemsukumia mwanasosholaiti Vera Sidika wimbo wa mahaba kutoka kwa albamu, Vee, aliyoitunga spesheli kwa ajili yake na amemchagulia wimbo unaokwenda na jina ‘Moyo Wangu’ na kuwatakia wote wenye wako katika mahusiano ya kimapenzi kusikiliza wimbo huo pia.

Mwanasosholaiti Vera amefurahia ujumbe huo wa Brown Mauzo kwake na akamjibu kimahaba mno

Awww my baaaaaby nakupenda,” alijibu Vera

Brown Mauzo anasema kwamba tangia siku ya kwanza Vera Sidika alitia nanga moyoni mwake, alijua huyu alikuwa ni mtu spesheli sana maishani mwake tangia mwanzo.

Amemsifia kwa kuwa mama mzuri kwa mwanao Asia na kusema kwamba katu hatosita kuikuza familia yao Pamoja.

Mapemzi mubashara!