Mulamwa bado anamiliki akaunti yangu ya Instagram- Carol sonie

Muhtasari

• Aliyekuwa mchumba wake mcheshi Mulamwa, Carol Sonie amekiri kwamba Mulamwa bado anamiliki akaunti yake ya Instagram.

• Aidha Sonie amesema kwamba kuna mambo mengi ambayo angependa kuyafichua ila wakati mwafaka ukifika basi atayaweka paruwanja kwa umma.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Aliyekuwa mchumba wake mcheshi Mulamwa, Carol Sonie amekiri kwamba Mulamwa bado anamiliki akaunti yake ya Instagram.

Akizungumza katika mahijiano na mwanablogu Mungai Eve, Sonie amesema kwamba ilimlazimu kufungua akaunti nyingine ya Instagram ili kuendelea kutangamana na wafuasi wake na hata kufanikisha shughuli zingine za kutangaza biashara mbalimbali katika akaunti hiyo.

Kulingana naye haelewi mbona bado Mulamwa amedinda na akaunti hiyo, ila amesema kwa sasa amefungua akaunti nyingine na  mashabiki wake wanaweza kufanya mawasiliano naye kupitia ukurasa huo.

Aidha Sonie amesema kwamba kuna mambo mengi ambayo angependa kuyafichua ila wakati mwafaka ukifika basi atayaweka paruwanja kwa umma.

Vilevile ametoa cheche kali kwa wale wote wanaosema kwamba mtoto wake sio wa Mulamwa na kusema kwamba wanafanana kama shilingi kwa ya pili.

Sonkie ambaye pia ni muigizaji amewaahidi mashabiki wake kwamba anaandaa kazi za maigizo ambazo zitapakuliwa katika akaunti yake ya YouTube.