Kibao cha Awinja 'Sio lazima' chapiku Views 1M chini ya siku 4

Jacky Vicky katika mahojiano na Massawe Japanni
Jacky Vicky katika mahojiano na Massawe Japanni

Ngoma ya muigizaji Jacky Vike almaarufu kama Awinja imepita views Zaidi ya milioni moja chini ya siku nne tangu aizindue na kuipakia kwenye mtandao wake wa YouTube

Ngoma hiyo ambayo inakwenda kwa jina ‘Sio Lazima’ mpaka sasa inazidi kuongoza kwenye charts za trending huku ikizidi kudedea nambari moja nchini Kenya katika mtandao wa YouTube kwa siku tatu mfululizo

Awinja aliizindua ngoma hii siku chache kabla ya siku kuu ya Valentino na maudhui yake ni kwamba anawashauri watu wasiokuwa na wa kuwasherehekea siku ya wapendanao kwamba si lazima.

Akizungumza katika mahojiano ya kituo kimoja cha redio, Awinja aliwasuta wakosoaji wake ambao waliibua hisia hasi kuhusu kujihusisha kwake katika Sanaa ya muziki na kusema kwamba lengo lake kuu katika Maisha ni kujiburudisha.

“Kelele ya chura haimzui ng’ombe kukunywa maji…nilisema as long as I’m having fun, iyo ingine hainihusu, lakini siezi wa-blame, sisi ni binadamu na kila mtu ana options zake especially when it comes to music, Awinja alisema.

Mafanikio haya makubwa ambayo hata yeye mwenyewe hakuyatarajia alisema yalimpa matumaini ya kujiunga katika Sanaa ya muziki siku za mbeleni hata kama bado kuna kiza.

“Nikitoka naingia kwa politics ndio ni ya kushtua lakini hii muziki bado iko kwa entertainment industry…It’s just one of those things nilijiambia nitajaribu siku moja nione. Sitaki kuzungumzia future, kitu najua ni leo, naeza wa-surprise, kesho sijui, sina habari na siwezi pangia,” alisema Awinja.

Muigizaji huyo anakuwa wa hivi punde kujiunga katika tasnia ya muziki baada ya wenzake kama vile Mammito Eunice, Diana B, Professor Hamo na Cartoon Comedian kuachila miziki yao ambayo inazidi kurindima na kutesa kwa vina vya tafsiri.

Hongera sana Awinja