Ulifukuzwa Konde Gang - Mwijaku amemvaa H-Baba

Muhtasari

• Mtangazaji na mwanamitindo wa kiume Mwijaku anayejulikana kama DC wa mtandao wa Instagram ameibuka na kuweka wazi kuhusu maneno ya msanii H-Baba aliyomwonya kukaa makini

• Ugomvi wa wawili hao umekua kwa Zaidi ya wiki moja sasa baada ya msanii H-Baba kupakia picha na video za Diamond katika kile alisisitiza kwamba ni kumpongeza

Mwijaku
Mwijaku
Image: instgram/mwijaku

Mtangazaji na mwanamitindo wa kiume Mwijaku anayejulikana kama DC wa mtandao wa Instagram ameibuka na kuweka wazi kuhusu maneno ya msanii H-Baba aliyomwonya kukaa makini kutokana na taarifa anazozisambaza kwamba Harmonize na H-Baba wamevuruga urafiki baada ya H-Baba ku unfollow Konde Boy kwenye Instagram.

Mapema Februari 15, H-Baba katika mahojiano na kituo cha Clouds alisema kwamba yeye na Harmonize ni Rafiki wa kitambo sana na katu hakuna mtu anaweza wachonganisha, na kumuona Mwijaku kukaa mbali na urafiki wao huo.

Mwijaku vile vile ametoka Februari 16 na kufanya mahojiano ambapo amemvaa H-Baba kwa kumwambia kwamba Konde Gang hawana haj ana yeye kwani walifanya kumpunguza tu kutokana na ukongwe wake.

Ugomvi wa wawili hao umekua kwa Zaidi ya wiki moja sasa baada ya msanii H-Baba kupakia picha na video za Diamond katika kile alisisitiza kwamba ni kumpongeza tu kutokana na ufanisi wake mkubwa wa kuwa mwanamuziki kutoka Afrika Mashariki kupiga show mubashara kwenye tamasha la Grammy.

Hapo ndipo mtangazaji Mwijaku alianza kumkejeli na kusema kwamba anajibeba kwa Diamond ili apewe dili Wasafi na eti ametimba maji kule Konde Gang, madai ambayo H-Baba aliyaweka wazi kwamba uswahiba wake na Harmonize bado upo na ulianza kitambo sana.