Akaunti ya YouTube ya Ochungulo family imedukuliwa

Muhtasari

• Akaunti ya YouTube ya kundi la muziki la Uchuongolo family imedukuliuwa na watu wasiojulikana huku hatua za kuirejesha zikiendelea.

• Kwa sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona iwapo akaunti hiyo itarejeshwa na mdukuzi huyo kupatikana na kueleza sababu zake za kufanya kitendo hicho.

Ochungulo family
Ochungulo family
Image: Instagram KWA HISANI

Akaunti ya YouTube ya kundi la muziki la Uchuongolo family imedukuliuwa na watu wasiojulikana huku hatua za kuirejesha zikiendelea.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Nameless amesema kwamba akaunti hiyo ambapo pia ngoma ya Bandana ya E Sir ilikuwa imepakuliwa imedukuliwa na kwamba kiwa ushirikiano na wasanii hao wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba wanaipata akaunti hiyo na hatua kuchukuliwa kwa aliyefanya kitendo hicho.

“Hamjambo ndugu zangu? Kwa bahati mbaya akaunti ya YouTube ya Uchuongolo family ambapo pia ngoma ya imedukuliwa Bandana ya E Sir ilikuwa imepakuliwa imedukuliwa. Nimefahamu hili kutoka kwa mashabiki ambao wamenipigia simu kuuliza mbona wimbo huo haupo mtandaoni. Tunafuatailia kujua tutafanyaje kurejesha akaunti hiyo na bila shaka tutawajulisha,” aliandika Nameless.

Hiki sio kisa cha kwanza cha akaunti za wasanii kudukuliwa, cha hivi punde kikiwa cha Diana B huku mashabiki wakitaka kufahamu sababu za wadukuzi hao kuwalenga watu mashuhuri na pia hatua kali kuchukuliwa kwao.

Kwa sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona iwapo akaunti hiyo itarejeshwa na mdukuzi huyo kupatikana na kueleza sababu zake za kufanya kitendo hicho.