Justina Syokau ametengana na 'mchumba' wake, Ringtone Apoko

Muhtasari

• Msanii wa miziki ya injili, Justina Syokau amesema kwamba ameachana rasmi na ‘mpenzi’ wake, Ringtone Apoko.

• Licha yake kudata kwa Ringtone, Syokau sasa anaonekana kuelekeza hisia zake kwa staa wa bongo, Rayvanny akisema kwamba angependa sana kuwa katika mahusiano naye.

 

Justina Syokau

Msanii wa miziki ya injili, Justina Syokau amesema kwamba ameachana rasmi na ‘mpenzi’ wake, Ringtone Apoko.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Mungai Eve, Syokau amesema kwamba penzi lake kwa msanii huyo limeisha baada yake kutupwa nje ya hafla ya kuzindua album ya Size 8.

Katika hafla hiyo, Ringtone alionekana akishikana mashati na Dj Mo, jambo ambalo Syokau amesema  lilionyesha udhaifu wake na kwamba hawezi akamkinga na maadui wake.

Aidha Justina Syokau amesema kwamba Ringtone alifanya kupiga magoti wakati ambapo alikuwa akiomba msamaha kwa watumishi wa Mungu waliokuwa katika hafla ile pamoja na Dj Mo, akisema kwamba hiyo ilikuwa njia moja ya kuabudu binadamu, jambo ambalo halitakikani kabisa.

Licha yake kudata kwa Ringtone, Syokau sasa anaonekana kuelekeza hisia zake kwa staa wa bongo, Rayvanny akisema kwamba angependa sana kuwa katika mahusiano naye.