Nimeokoka, huu mwaka nataka kubatizwa! - Kartelo

Muhtasari

• Mchekeshaji na msanii Kartelo ameweka wazi malengo yake ya mwaka huu na miongoni mwao ni kubatizwa kwa sababu alishaokoka.

Kartelo
Kartelo

Mchekeshaji na msanii Kartelo ameweka wazi malengo yake ya mwaka huu na miongoni mwao ni kubatizwa kwa sababu alishaokoka.

Akizungumza na Mungai Eve, Kartelo alisema kwamba ameokoka na anatarajia kubatizwa mwaka huu kwani Yesu ni mwokozi wake.

“Mi hukuwa mtu wa church tangu kitambo. Saa hii nimeokolewa. Yesu ni Mwokozi. Huu mwaka, nataka kuwa baptized,” alisema Kartelo.

Mchekeshaji huyo ambaye alivuma sana kati yam waka 2019 na 2020 alipoulizwa ukimya wake kutoka kwenye mitandao ya kijamii alisema kwamba ni uamuzi wa kibafsi na alifanya hivo ili kujipatia muda Zaidi wa kujitathmini.

"Nafocus na vitu personal kama familia, mamorio, spiritual growth na project zangu personal. Kutumia mokoro pesa sio enough," alisema Kartelo.

Kartelo ambaye kwa muda mrefu ametajwa kuwa na ugomvi wa chini kwa chini na mchekeshaji mwenza Chipukeezy pia alifichua kwamba amemsamehe na hana beef na yeye na kusema kwamba yuko tayari kufanya kazi pamoja na Chipukeezy kama itatokea na aone inamfaidi.

“Mimi namrespect sana kwa sababu Chipukeezy amenivusha daraja mingi sana na tumeokoleana sana. Tumejengana sana na amenisaidia sana. Out of hiyo respect, siwezi kuwa na chuki na yeye. Mimi siwezi kosa ku work na yeye na that’s if mtu ako willing tutafanya kazi,” alisema Kartelo.