"Shukran Mama Mueni!" Bahati amsifia baby mama wake Yvette kwa kurahisisha uzazi wenza

Muhtasari

•Wapenzi hao wawili wa zamani walihudhuria hafla ya kuhitimu iliyofanyika shuleni na kumsherehekea binti yao kwa mafanikio yake ya kielimu.

•Bahati alimshukuru Yvette kwa  kufanya ushirikiano katika malezi ya binti yao kuwa rahisi licha ya tofauti zao za hapo awali.

Image: INSTAGRAM// BAHATI KENYA

Siku ya Ijumaa ilikuwa maalum sana kwa bintiye Bahati na aliyekuwa mpenzi wake Yvette Obura, Mueni Bahati.

Mueni ambaye ana umri wa miaka sita  alisherehekea kuhitimu kutoka shule ya awali na kujiunga rasmi na shule ya msingi.

Licha ya kutengana miaka mingi iliyopita, wapenzi hao wawili wa zamani walihudhuria hafla ya kuhitimu kwa binti yao iliyofanyika shuleni yao ya Tender Care Junior Academy na kumsherehekea kwa mafanikio hayo yake ya kielimu.

"Siku ya binti yetu (pre-graduation) Tunamshukuru Mungu kwa umbali tuliofika" Yvette aliandika chini ya picha ya hafla hiyo ambayo alipakia Instagram.

Bahati ambaye kwa sasa yuko katika ndoa na Diana Marua alimtakia baraka tele mpenzi huyo wake wa zamani pamoja na binti yao.

Mwanamuziki huyo sifika alimshukuru Yvette kwa  kufanya ushirikiano katika malezi ya binti yao kuwa rahisi licha ya tofauti zao za hapo awali.

"Sasa nahudhuria sherehe ya kuhitimu kwa binti yangu kutoka shule ya awali. Shukran Mama Mueni kwa kufanya uzazi wenza wetu kuwa rahisi! Mungu wangu akubariki na abariki binti yetu Mueni Bahati" Bahati aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hapo awali mke wa sasa wa Bahati, Diana Marua alimsherehekea Mueni kwa kupiga hatua hiyo ya kielimu.

Diana ambaye hivi majuzi alizindua taaluma yake ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B alisema anajivunia binti huyo wa kwanza wa mumewe.

"A Girl Toto, mtoto wa malkia @mueni_bahati anahitimu leo. Hongera sana mtoto wa kike, tunajivunia wewe. Hugs na mabusu kutoka kwa Aunty Dee" Diana aliandika.

Bahati na Yvette walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka kadhaa iliyopita kabla ya kutengana kwao. Hata hivyo wameendelea kushirikiana vizuri katika malezi ya binti yao.