Jux kumtuza laki moja atakayebashiri siku na muda wa video yake na Gykie itatoka

Muhtasari

• Juma Jux ametangaza zawadi ya laki moja za Kitanzania kwa atakayebashiri sahihi tarehe na  muda ambao video ya collabo yake na Mghana Gykie itatoka.

Juma Jux
Jux, Gykie Juma Jux
Image: Instagram

Mwimbaji matata wa bongo fleva, Jums Jux ametoa ahadi ya kutoa zawadi ya shilingi laki moja za Tanzania kwa shabiki wake yeyote mwenye atagonga ndipo katika kubashiri kwa usahihi ni siku gani na saa ngapi video ya collabo yake na Mghana Gyakie itatoka.

 Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mwanafasheni wa kiume alisema kwamba ngoma yake na msanii Gyakie kutoka Ghana ambayo waliibatiza kwa jina ‘I Love You’ iko tayari na kudokeza kwamba itatoka wiki kesho ila akawapa changamoto wafuasi na mashabiki wake kubashiri tarehe kamili na muda ili kujishindia zawadi hiyo ya laki moja.

My amazing fans, Wiki ijayo nina jambo lenu nalileta mjini. Tanzania x Ghana  Video yangu ya wimbo wangu na @Gyakie_ #ILoveYou iko tayari, Itatoka wiki ijayo. Ninachohitaji kutoka kwako ni kuniambia hiyo video nitaitoa lini na saa ngapi? Ukipatia siku na saa ya kutoka video ya #ILoveYou utafurahia, nina zawadi yako ndogo ya Shillingi Laki Moja. Let's get busy my people. Comment ukianzia na haghtag #JuxGyakieILoveYou. Date/Day/Time,” aliandika Jux kwenye Instagram yake.