"Mimi na Jemutai tanalea watoto tu!" Profesa Hamo akana ndoa na Jemutai

Muhtasari

•Mchekeshaji huyo alisema waliafikiana na Jemutai kushirikiana katika malezi ya watoto wao wawili baada ya ndoa kushindikana.

•Hamo amesema kuwa hajamkazia Jemutai kwa namna yoyote ile na amempa uhuru wa kuishi maisha yake jinsi atakavyo bila kumfuatilia.

Image: INSTAGRAM// PROFESA HAMO

Mchekeshaji mashuhuri Herman Kago almaarufu kama Profesa Hamo amekana ndoa yake na mchekeshaji mwenzake Stella Bunei. (Jemutai)

Akiwa kwenye mahojiano na Tuko Extra, Hamo alieleza kuwa uhusiano wake na Jemutai ni uzazi tu ila sio ndoa.

Mchekeshaji huyo alisema waliafikiana na Jemutai kushirikiana katika malezi ya watoto wao wawili baada ya ndoa kushindikana.

"Mimi na Jemutai tunalea watoto tu pamoja. Niko na mke na Jemutai ambaye tunalea watoto pamoja. Baaada ya kushiriki mazungumzo tuligundua kuwa kuna mambo ambayo hatuwezi kubadilisha. Lakini kuna kitu tulicho nacho, watoto wazuri. Badala ya kufanya mambo ambayo yameshindikana, tuliona kuna kitu ambacho kinafanya kazi, tuko na watoto. Tulikubaliana kuwalea," Hamo alisema.

Ameweka wazi kuwa mkewe hana tatizo lolote kwake kushirikiana na Jemutai katika malezi  ya watoto wao na amekuwa akiunga mkono mpango huo.

Hamo amesema kuwa hajamkazia Jemutai kwa namna yoyote ile na amempa uhuru wa kuishi maisha yake jinsi atakavyo bila kumfuatilia.

"Kila mtu anajua nafasi yake. Najua jinsi ya kusawazisha majukumu yangu, najua jinsi ya kuwa na watoto wangu. Najua namna ya kuwaongelesha wakati siko karibu. Najua namna ya kupatia Jemutai uhuru wa kuishi maisha yake. Namuunga mkono kikamilifu," Hamo alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwamazingira ambayo ameweza kujenga yamempa raha kubwa. Aidha amesisitiza kuwa  anajivunia watoto wake na Jemutai sana.