'Umepigana vita kwa ajili yangu,'Grace Ekirapa amsherehekea dada yake

Muhtasari
  • Grace Ekirapa ni miongoni mwa watangazaji wanaosherehekewa sana nchini na wanamitandao
grace ekirapa
grace ekirapa

Grace Ekirapa ni miongoni mwa watangazaji wanaosherehekewa sana nchini na wanamitandao.

Grace anatarajia mwanawe wake wa kwanza na mumewe muigizaji Pascal Tokodi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisherehekea siku ya kuzaliwa ya dada yake kwa ujumbe maalum.

Grace alimlimbikizia sifa dada yake huku akisema kwamba amepigana vita kwa ajili yake, na kumtetea mahali hangeweza kujitetea.

"Kwa mzaliwa wetu wa mwisho ambaye anakataa kutenda kama mmoja. Wewe ni gem katika maisha yangu. Umenipigania vita, umenitetea mahali nisingeweza kufanya mwenyewe, umenishika mkono na kunisaidia kuinuka nilipodhani nitazama na bado unafanikiwa kuwa peke yangu unaniudhi,

@juliet.ekirapa nakupenda sana na naomba Mungu atulinde milele na kama sivyo basi atuvushe pamoja maana siwezi kuona maisha yangu bila wewe. Ninasherehekea mwanamke mwenye nguvu ambaye umekuwa.

Jinsi unavyorudi nyuma kutoka kwa misimu migumu ni kitu ninachovutiwa nawe na ninakuombea mtoto wangu akope baadhi ya sifa zako ili niwe na ukumbusho wako kila wakati nyumban,Happy Birthday Dada yangu Mdogo. Nakupenda."