Carrol Sonie azawadiwa bima ya matibabu ya 1.2M, Mulamwah hashughukilii mtoto

Muhtasari

• Baada ya kufichua kwamba Mulamwah hamshughulikii mtoto, Carrol Sonie amezawidiwa bima ya matibabu yenye thamani ya 1.2M  ili kusimamia matibabu yake na mtoto.

Carrol Sonie na mwanawe Keilah
Image: Instagram

Carrol Sonie ametema nyongo na kusema kwamba Mulamwah hajawahi shughulikia mwanawe Keilah licha ya kutomnyima nafasi ya kumuona na kumshughulikia kama ambavyo mchekeshaji huyo alivyodai katika mahojiano ya hivi karibuni.

Sonie aliambia Dr. Ofweneke kwamba hajawahi kumzuia Mulamwah kuona mtoto wao na kwamba mchekeshaji huyo hajawahi shughulikia malezi yam toto wao tangu watengane mwishoni mwa mwaka jana.

Alipoulizwa kama wanashirikiana katika uzazi, Sonie alikataa na kusema ni yeye tu humshughulikia mtoto.

“Ni mimi na mtoto wangu tu hata kama sijawahi mzuia kuona mtoto,” alifichua Sonie.

Pia alifichua kwamba mtoto alikuwa mgonjwa na ni yeye pekee anamshughulikia jambo ambalo lilimgusa Ofweneke na kumpa zawadi mbalimbali zikiwemo bima ya matibabu yenye thamani ya milioni 1.2 za kenya na vocha ya shilingi elfu nane za matumizi ya kimsingi ya mtoto.

Kuvunjika kwa mahusiano ya wawili hao kumekuwa kikichafua mitandaoni huku wote wakitupiana lawama mpaka kuwaweka watu katika njia panda wasijue ni nani aliyekuwa mwenye makosa mpaka kupelekea kuvunjika kwa mahusiano yao.