Uzuri wazungu hawaangalii sura, wanaangalia tabia na roho- Nyota Ndogo

Amewasuta wanamitandao wanaokosoa sura na maumbile yake.

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto wawili amekuwa kwenye ndoa na mzungu kutoka Udenmarki, Henning Nielsen kwa zaidi ya miaka mitano.

Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla almaarufu Nyota Ndogo amewasuta wanamitandao wanaokosoa sura na maumbile yake.

Msanii huyo kutoka eneo la Pwani alikosolewa na baadhi ya mitandao baada ya kupakia video inayoonyesha mwonekano wake kabla na baada ya kupaka make up usoni.

Kufuatia hayo Nyota Ndogo alipakia video yake nyingine akiashiria kuwa anajivunia mwonekano wake na anajiamini.

"Uzuri wa wazungu hawaangalii sura, wanaangalia tabia na roho ya mtu," Nyota Ndogo aliandika chini ya video hiyo.

Mama huyo wa watoto wawili amekuwa kwenye ndoa na mzungu kutoka Udenmarki, Henning Nielsen kwa zaidi ya miaka mitano.

Wawili hao wamekabiliana na ukosoaji mkubwa kuhusiana na ndoa hiyo yao ila hawajakubali itikisike.

Baadhi ya mashabiki wa msanii huyo walijitokeza kutoa hisia mbalimbali kuhusiana na ujumbe huo wake uliolekezwa kwa wakosoaji wa mwonekano wake.

@behatibey Nyota wewe ni mzuri kwa kuwa Mungu alikuumba kwa mfano wake. Kuna binadamu yu aweza umba mtu hapo wa mguu mmoja?

@marychacha_store Wewe ni mrembo sana.. ndani na nje, kila wakati.

@jasmin_online_store Uko mrembo mamas, mbona uko mzuri aki.

@jaynemachocho Sipendi hiyo caption, unafaa kuamini kuwa wewe ni mrembo.

@yusra_almendhry Hujiamini tu.