Baada ya kuzama kwa muda mrefu, hatimaye Churchill show imepata makao mapya ndani ya runinga ya TV47.
Hii ni baada ya kutamatisha mkataba wake na runinga ya NTV ambao umedumu kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo mashabiki wamekuwa wakipokea Burudani kutoka kwa wacheshi mbalimbali.
Kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, Churchill alisema kwamba imekuwa safari yenye changamoto, faida na mafunzo si haba huku akishukuru kila mmoja ambaye alitoa mchango kuhakikisha anaafikis ndoto yake ya kukuza vipaji na kuburudisha Wakenya.
"Imekuwa zaidi ya miaka kumi si ndio? Hiyo stori tutaitoa wakati MWENGINE," Churchill alisema.
Aidha, alisema kwamba anafurahi kwamba hatimaye wamepata makao mapya na kuwahakikishia mashabiki kwamba watazidi kupokea burudani Kali.
Pia alishukuru usimamizi wa TV47 kwa kumpa jukwaa na kuaminia kazi yake, huku akiahidi kuchapa kazi ili kuinua viwango vya stesheni hiyo hata zaidi.
Baadhi ya wacheshi Kama vile Sleepy David alionyesha furaha yake kwenye mitandao, huku aliwataka mashabiki kuwa tayari kwani wameandaa bonge la shoo, kuanzia tarehe 19 mwezi huu wa Machi.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wanahisi kwamba Churchill alichukua hatua mbaya ikilinganishwa kwamba NTV ilikuwa katika viwango vya juu zaidi kuliko TV47.
Kwa Sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona kipindi hicho kitafanya vipi pindi kitakapoanza kuruka hewani moja kwa moja.