"Nimelazwa hospitali mara kadhaa!" Nadia Mukami afunguka kuhusu safari yake ngumu ya ujauzito

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo amefichua kuwa amekumbana na changamoto kadhaa zikiwemo upungufu wa damu mwilini na kutapika kupita kiasi.

•Nadia aliweka wazi kuwa mume wake Arrow Bwoy amekuwa nguzo muhimu sana katika safari yake ya ujauzito.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Nadia Mukami na Arrow Bwoy

Malkia wa muziki wa kisasa Nadia Mukami amesema kuwa safari ya ujauzito wake haijakuwa rahisi hata kamwe.

Nadia amesema alichelewa kutangaza habari za ujauzito wake kwa kuwa alikuwa anasubiri wakati mwafaka ambao atakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Mwanamuziki huyo amefichua kuwa amekumbana na changamoto kadhaa zikiwemo upungufu wa damu mwilini na kutapika kupita kiasi.

"Ujauzito sio rahisi. Mimi nilikuwa na upungufu wa damu, hiyo ndiyo changamoto kuu. Nilikuwa nashindwa kukula juu ya kutapika kupita kiasi. Nimelazwa hospitalini mara kadhaa. Sababu kwa nini sikutaka kusema ni kuwa nilitaka kuwa sawa kabla ya kuambia dunia kuwa natarajia mtoto.Hakuna kitu kama kuficha mimba. Lazima mtu asubiri mpaka awe tayari," Nadia alisema akiwa kwenye mahojiano na Eve Mungai.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 25 pia alifichua kuwa ujauzito ulisababisha mabadiliko makubwa muonekano wake.

Nadia aliweka wazi kuwa mume wake Arrow Bwoy amekuwa nguzo muhimu sana katika safari yake ya ujauzito.

"Amekuwepo katika mazuri na mabaya. Hajawahi kosa kuenda nami kliniki. Kuna wakati niliamka mhemko wa hisia nikamwambia nitajipeleka hospitali. Alinitoka nikadhani ameenda. Nilimpata hospitalini. Najivunia usaidizi wake. Amekuwepo kwa ajili yangu," Nadia  alisema.

Arrow Bwoy kwa upande wake alisema kuwa anasubiri sana kumkumbatia mtoto wao mikononi. Alisema anajivunia kusaidia mke wake licha ya kuwa walipoteza ujauzito wao wa kwanza.

Alifichua kuwa mkewe alimshinikiza sana ampachike ujauzito  kwa kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kupata mtoto.

Mapema mwaka uliopita wanandoa hao walipoteza ujauzito wao wa kwanza ukiwa bado mchanga.