"Hawa ndio walinishika mkono nikianza," Erick Omondi

Muhtasari

• Mcheshi Erick Omondi ametaja vigezo alivyotumia kuwateua watu waliohudhuria sherehe yake ya kuzaliwa.

• “…Kama Churchill ni babangu, alinisaidia nilipoanza safari hii,” Omondi alisema.

Eric Omondi
Image: Instagram

Mcheshi Erick Omondi ametaja vigezo alivyotumia kuwateua watu waliohudhuria sherehe yake ya kuzaliwa.

Akizungumza na wanablogu, Omondi alisema kwamba alizingatia watu muhimu katika maisha yake na ambao wamempa sapoti katika safari yake ya ucheshi.

“…Kama Churchill ni babangu, alinisaidia nilipoanza safari hii,” Omondi alisema.

Aidha, Omondi alisema sababu ya kutoweka bango la Bahati mitandaoni ni kutokana na ugomvi kati yake na Willy ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.

 Alimtaja mwanasosholaiti Amberay kuwa rafiki yake wa karibu na ambaye wamefanya kazi nyingi pamoja.

Erick alisisitiza kwamba ataendelea kupigania kuchezwa kwa asilimia 75 ya muziki wa Kenya, na kwamba atashurutisha vyombo vyote vya habari kufuata mkondo huo.

Alionyesha imani yake kwa wabunge, ambao alisema kwamba lazima watapitisha mswada huo.

Omondi pia alisema kuna mikakati kuandaa shoo kubwa hapa Kenya ambapo atawaburudisha mashabiki wake.