EP ya Diamond ni mbaya, aliharibia watu usingizi - Mwijaku

Muhtasari

• Mwanahabari kutoka Tanzania, Mwijaku ameisuta EP ya Diamond Platinumz akisema kwamba msanii huyo aliwaharibia mashabiki wake usingizi.

• “Mwambino ameshindwa kuimba kwa kweli, akaachie wale wanaojua kufanya hizi kazi,” Mwijaku alisema.

 

Mwijaku
Mwijaku
Image: instgram/mwijaku

Mwanahabari kutoka Tanzania, Mwijaku ameisuta EP ya Diamond Platinumz akisema kwamba msanii huyo aliwaharibia mashabiki wake usingizi.

Akizungumza kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, Mwijaku alisema kwamba EP hiyo sio kali kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakitarajia hata baada ya kuisubiria kwa muda mrefu.

Aidha alisema kwamba Diamond ameshindwa kuimba na hivyo kumtaka aachane na muziki na kujishughulisha na mambo mengine.

“Mwambino ameshindwa kuimba kwa kweli, akaachie wale wanaojua kufanya hizi kazi,” Mwijaku alisema.

Mwijaku alitupa vijembe akisema kwamba Simba anapaswa kuiga mfano kutoka kwa Alikiba na Harmonize ambao anaamini wanajua kutengeneza miziki mizuri.

 Aliweka wazi kwamba ngoma ya Harmonize itakuwa inatoka tarehe 12/3/2022 kama njia moja ya kutoa upinzani kwa EP yake Diamond Platinumz.

Ikumbukwe kwamba katika siku za hivi karibuni tulimuona Mwijaku akipata ubalozi katika kampuni ya Wasafi bet ila anaonekana kushikilia msimamo wake wa kuwa upande wa Harmonize.