"Ruto na Odinga mna siku saba kunitafuta," - Erick Omondi

Muhtasari

• Mcheshi Erick Omondi ametoa makataa ya siku saba kwa Raila Odinga na William Ruto kumtafuta na kumwelezea mipango yao kwa vijana wa taifa hili.

• “Tumechezewa sana, 2017 uhuru alikuwa na Ruto sasa yuko na Raila Odinga, kwa nini kila wakati lazima iwe watu wawili tu ambao lazima wawe uongozini?” alisema Omondi.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Erick Omondi

Mcheshi Erick Omondi ametoa makataa ya siku saba kwa Raila Odinga na William Ruto kumtafuta na kumwelezea mipango yao kwa vijana wa taifa hili.

Kupitia video aliyopakia katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema kwamba viongozi hao wamekuwa wakitumia mbinu zilezile kuwadanganya vijana.

“Tumechezewa sana, 2017 uhuru alikuwa na Ruto sasa yuko na Raila Odinga, kwa nini kila wakati lazima iwe watu wawili tu ambao lazima wawe uongozini?” alisema Omondi.

Amekashifu hatua ya Uhuru Kenyatta na idadi kubwa ya viongozi wakuu serikalini kuunga mkono Raila Odinga kuwa rais katika uchaguzi mkuu ujao akisema kuwa huo ni ukoloni mamboleo na kwamba wakenya wanapaswa kupewa nafasi ya kuchagua kiongozi wao.

Alisema kwamba idadi ya vijana nchini ni asilimia 63 na hivyo basi wanapaswa kujumuishwa vilivyo katika mipango ya serikali ili kuhakikisha maisha yao yanaboreshwa.

Amewataka vijana kuungana na kuzungumza lugha moja ili kuchagua kiongozi ambaye atashughulikia mahitaji yao kikamilifu.