KRG the Don azungumzia ugomvi wake na Redsan

Muhtasari

• Mwanamuziki KRG the Don ametaja sababu za ugomvi kati yake na msanii Redsan.

• “Nilikuwa nimependa ngoma moja kwa album yake, nikasema nitasimamia uzalishaji wa video hiyo,” KRG alisema.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: KRG the Don

Mwanamuziki KRG the Don ametaja sababu za ugomvi kati yake na msanii Redsan.

Akizungumza katika mahojiano na Obinna tv, KRG alisema kwamba Redsan alimkosea heshima na kukosa kuona umuhimu wake katika gemu la burudani.

KRG alisema kwamba alikuwa amependa wimbo mmoja kwenye album ya Redsan na kujitolea kugharamikia uzalishaji wa kibao hicho maadamu wataje kampuni yake ya Fast Cash Music kwenye video hiyo.

“Nilikuwa nimependa ngoma moja kwa album yake, nikasema nitasimamia uzalishaji wa video hiyo,” KRG alisema.

Kulingana na KRG, baadaye waliokuwa wanahusika katika mchakato wa kuhariri video hiyo, waliweka jina la kampuni ya Sonny badala ya jina la kampuni yake, jambo ambalo lilimkera sana.

Aidha alizungumzia kuhusu kudhalilishwa hewani katika mahojiano kwenye kipindi cha Trend katika runinga ya NTV ambapo kulingana naye, Redsan na Amina walishirikiana kumkosea heshima.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba alitoa onyo kwa kipindi hicho kutocheza ngoma zake tena, kwa madharau waliyomuonyesha.