Diamond azungumzia suala la Zuchu kumweka kwenye wallpaper ya simu yake

Muhtasari

• Diamond alisema kuwa hatua hiyo iliashiria kuwa Zuchu anathamini kazi yake kama bosi wake katika WCB.

•Staa huyo ambaye hivi majuzi aliachia EP mpya 'FOA' aliweka wazi kuwa yeye amesave Zuchu kama 'Zuu' kwenye simu yake.

Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: HISANI

Bosi wa WCB Diamond Platnumz amefurahia hatua ya msanii wake Zuchu kumsave kwa jina tamu kwenye simu yake na kuweka wallpaper ya picha yake.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Diamond alisema kuwa hatua hiyo iliashiria kuwa Zuchu anathamini kazi yake kama bosi wake.

Diamond alisema kuwa hilo ni jambo la kawaida na haimaniishi kwamba wako kwenye mahusiano.

"Unapokuwa kiongozi unahifadhiwa kwa majina tofauti. Mimi kama kiongozi wake wa taasisi, hakuna ubaya yeye kuniweka katika DP. Kama kweli alikuwa ameniweka, nami nafaa nimshukuru sana. Inaonyesha anathamini juhudi ambazo naweka  katika taaluma yake," Diamond alisema.

Staa huyo ambaye hivi majuzi aliachia EP mpya 'FOA' aliweka wazi kuwa yeye amesave Zuchu kama 'Zuu' kwenye simu yake.

Zuchu alipokuwa katika studio za Wasafi mwezi jana picha za Diamond zilionekana kwenye wallpaper ya simu  yake.

 Wakati ule alisisitiza kuwa hatua yake hakikumaanisha kuwa ana hisia za kimapenzi kwa bosi wake Diamond Platnumz.