"Sisi sio ma-ex wenye chuki" Zari azungumzia uhusiano wake wa sasa na Diamond Platnumz

Muhtasari

•Zari anasema kuwa yeye na Diamond ni marafiki wakubwa na hakuna uhasama wowote kati yao licha ya kuwa mahusiano yao yaligonga ukuta.

•Zari pia anakiri kuwa amewahi kuvunjwa moyo mara nyingi na amekumbana na changamoto si haba hapo awali.

Zari Hassan na Diamond Platnumz
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri kutoka Uganda ,Zari Hassan ni mmoja wa watu mashuhuri ambao wameshirikishwa kwenye shoo ya 'Young, Rich & Famous' ambayo inatarajiwa kuachiliwa siku ya  Ijumaa (Machi 18, 2022}.

Katika shoo hiyo, wasanii walioshirikishwa wanatarajiwa kuzungumzia na kuonyesha mambo mbalimbali kuhusiana na maisha yao.

Zari atashiriki jukwaa moja na mpenzi wake wa zamani na baba ya watoto wake wawili Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz. 

Katika kipande kidogo cha shoo hiyo ambacho alipakia Instagram,  Zari anasikika akizungumzia kazi zake na uhusiano wake wa sasa na Diamond.

Mama huyo wa watoto watano anajimbulisha kama mwanamke anayetia bidii kubwa  wazi kazini ili kupata chochote anachotamani.

"Mimi ni Boss Lady ambaye hufanya kazi kwa bidii na huwa napata chochote ambacho huwa nataka kwa kuwa huwa natia bidii.Mimi pia ni mama. Niko na watoto watano, watatu nilipata na mpenzi wangu wa zamani na wawili nilipata na Diamond," Zari anasikika akisema.

Mwanasoshalaiti huyo ambaye kwa sasa anaishi Afrika Kusini anaendelea kuzungumzia uhusiano wake na mzazi mwenzake Diamond.

Zari anasema kuwa yeye na Diamond ni marafiki wakubwa na hakuna uhasama wowote kati yao licha ya kuwa mahusiano yao yaligonga ukuta.

"Mimi na Diamond ni marafiki. Sisi sio wapenzi wa zamani wenye kinyongo. Sisi ni kama marafiki," Zari anasema.

Katika video hiyo, Zari pia anakiri kuwa amewahi kuvunjwa moyo mara nyingi na amekumbana na changamoto si haba hapo awali.