Erick Omondi amzindua Wanjigi kuwania urais

Muhtasari

• Erick Omndi amesema kwamba Wanjigi ndiye chaguo bora la kuongoz ataifa hili.

• Alishikilia kwamba taifa linahitaji uongozi mpya ambao utawahudumia wananchi.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Erick Omondi

Mcheshi Erick Omondi hatimaye amemzindua mfanyibiashara Jimmy Wanjigi kama mgombea faafu wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Agosti 9.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema kwamba Wanjigi ndiye kiongozi ambaye anaweza kulikomboa taifa hili.

Omondi alisema kwamba Wanjigi ana maono makubwa ambayo yanaweza kubadilisha hali ya uchumi ya taifa hili.

Haya yanajiri wakati ambapo chama cha Safina ambapo Wanjigi ni mwanachama, kinatarajiwa kuandaa mkutano wa wajumbe wiki hii ili kujadili kuhusu mikakati yao mbele ya uchaguzi mkuu.

Ifahamike kwamba mcheshi huyo alikuwa ametoa siku saba kwa Ruto na Raila kumtafuta ili wafanye mazungumzo, la sivyo atachukua hatua ambayo itabadilisha siasa za Kenya na kuhakikisha wawili hao hawashindi uchaguzi.

Kwa muda sasa, amekuwa akiwarai vijana kuungana na kumchagua kiongozi anayefaa kwani wanajumuisha asilimia kubwa ya wapiga kura hivyo wanaweza kufanya uamuzi wa kiongozi atakayeingia madarakani.