Nilikuwa nimelewa! Huddah atetea ujumbe wake kuhusu ex wake kusoma 'katiba'

Muhtasari

• Mwanasosholaiti huyo alijitetetea akisema kwamba alikuwa amelewa akichapisha ujumbe huo.

• Hii ni baada ya kusema kwamba wapenzi wake wote wa awali walikuwa wanajua kusoma katiba.


Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Huddah Monroe

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Huddah Monroe amejitokeza na kujitetea kuhusu ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram kuhusu wapenzi wake wa awali kuwa stadi katika kushiriki ngono.

Huddah alisema kwamba alikuwa amelewa kipindi anachapisha ujumbe huo mtandaoni, na kuwataka mashabiki wake kumsamehe.

Alisema kwamba mara kadhaa kipindi cha nyuma alipokuwa akitrend, ilikuwa baada ya kuchapisha ujumbe tatanishi akiwa mlevi.

"...Nilikuwa natrend kwa sababu ya kuumia simu nikiwa mlevi," Huddah alisema.

Aidha, alisema kwamba anachukia simu yake akiwa mlevi kwa sababu mara si moja hali hiyo imempelekea kujikuta matatani na kupokea matusi kutoka kwa mashabiki na washikadau mbalimbali.

Ikumbukwe kwamba, Huddah alikuwa amechapisha ujumbe kwamba wap[enzi wake wa awali walikuwa wasomaji wazuri wa 'katiba' na kujisifia kwa ueledi wake wa kuchagua wanaume wazoefu katika sekta hiyo.

Baadhi ya mashabiki walimkashifu vikali wakisema kwamba alikuwa anatafuta kiki ili apate umaarufu na azidi kuzungumziwa.