Tafuta kienyeji yako uing'arishe, Man Kush awaambia wanaume

Muhtasari

• Mhubiri Man Kush awataka wanaume kuwatunza wachumba wao.

• Amewaonya dhidi ya kutafuta wanawake warembo kabla hawajatafuta na kupata hela za kutosha.

Mhubiri Man Kush amewashauri wanaume kutafuta wachumba wa mashambani na kuwang'arisha iwapo wanataka ndoa zao kudumu.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Mungai Eve, Man Kush alisema kwamba mwanaume anapompata mwanamke ambaye bado hajafahamu ujanja wa mjini, inakuwa rahisi kwake kumnoa anavyotaka yeye.

"...Kama unataka kupata mwanamke mzuri tafuta yule wa mashambani, sio hawa wa mjini," Man Kush alisema.

Alisema kwamba wanawake wengi wa mjini washapitia mambo mengi na kuishi nao inahitaji gharama kubwa.

Vilevile aliwataka wanaume kuhakikisha wanatenga muda wa kuwapeleka wake zao katika likizo za kujivinjari, kama njia moja ya kuifanya ndoa iwe ya furaha.

Man Kush alikiri kwamba ni rahisi kwa mwanaume  kuishi na mwanamke ambaye ameanza naye  

Aidha, aliwataka wanaume kutafuta hela kwanza kabla hawajawazia kuingia katika mahusiano.

Alisema kwamba licha ya kuwa mhubiri, anatambua umuhimu wa pesa katika kufanikisha mambo mbalimbali maishani.

Ifahamike kwamba mhubiri huyo amedumu katika ndoa kwa zaidi ya miaka 30, huku akiwataka watu kuamini maneno yake kwani anazungumzia hali halisi ya kimaisha.