Mpenzi wa Stivo Simple Boy azamia pombe baada ya kuachwa

Muhtasari

• Mpenzi wa Stivo Simple Boy aonekana kwenye video akicheza densi ya wimbo wa kulewa huku akibugia kinachodhaniwa kuwa pombe.

Mpenzi wa Stivo, Pritty Vishy
Mpenzi wa Stivo, Pritty Vishy
Image: screengrab , Nairobi Gossip

Mpenzi wa msanii Stivo Simple Boy aliyedai kuachwa na msanii huyo, Pritty Vishy ameonekana kwenye video akiwa anacheza densi na chupa inayodhaniwa kuwa ya pombe mkononi, huku wimbo ukiimba kwamba ameachika sasa hana budi kulewa.

Katika video hiyo ambayo imesambazwa mitandaoni, Vishy anaonekana akicheza kwa ngoma hiyo yenye amaudhui ya kulewa kwa sababu ya kuachika.

Juzi mwanadada huyo alipakia video kwenye Instagram yake akilia kwa kile alikuwa anadai kwamba amenyang’anywa mpenzi wake Stivo na mwanamuziki Adasa kutokea pwani.

Simple Boy Jumatano aliweka wazi kwamba ni kweli uhusiano wake na Pritty  Vishy umefikia kikomo na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mapya bila uwepo wake.

“Nimeachika jamani niacheni nilewe,” wimbo huo ambao anaonekana akiusakatie na kunengua kwa mauno yake ya kutamanisha unaisikika ukiimba.

Watu wengi bado wanahisi hii ni kiki wanafukuzia huku baadhi wakisema kwamba huenda msanii Stivo Simple Boy na msanii mwenza Adasa wanafanya upishi wa collabo yao na ni mchezo tu ambao watatu hao wanacheza ili kuvutia ufuatiliaji mkubwa wa mitandaoni.