KRG awataka wanawake kukoma kutumia picha zake kujiridhisha kimwili kukoma, ni mfungo wa Ramadhani

Muhtasari

• “Kwa wanawake wote ambao mnamtolea macho ya tamaa ya kimapenzi Bughaa, tafadhali mwezi huu ni tofauti msitumie picha zangu au hata kunifikiria mkipiga punyeto kwa sababu mimi ninafunga" - KRG.

KRG the Don
KRG the Don
Image: Instagram

Msanii mtata nchini Kenya KRG the Don ametoa onyo kali kwa wanawake wote wanaomtolea mimacho kwa kumtamani.

KRG amewaonya wanawake hao kwamba mwezi huu ni tofauti sana kwani yeye anafunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na hataki kuamka asubuhi akiwa anajihisi na uchovu kutokana na wanawake hao kumfikiria au hata kuzitumia picha zake wakipiga punyeto.

“Kwa wanawake wote ambao mnamtolea macho ya tamaa ya kimapenzi Bughaa, tafadhali mwezi huu ni tofauti msitumie picha zangu au hata kunifikiria mkipiga punyeto kwa sababu mimi ninafunga. Sitaki kuamka asubuhi na uchovu… tafadhali,” alitoa onyo hilo kwenye Instagram yaker KRG.

Msanii ambaye kwa jina ya majazi anajiita Bughaa amekuwa katika siku za hivi karibuni na utata mkubwa haswa baada ya kutangaza kwamba aliamua kumuacha mke wake kwa sababu aligundua anatembea na watu wa chini aliowalinganisha kama chokoraa.

Amekuwa akijaajaa mitandaoni huku akipapurana na baadhi ya watu mashuhuri likiwemo kundi la gengetone la Mbogi Genje na mkuza maudhui kwenye YouTube, Andrew Kibe miongoni mwa watu wengine.