Janet Otieno amtambua Ringtone kama 'chairman' wa Gospel

Muhtasari

• Msanii Janet Otieno ameweka wazi kwamba anamtambua Ringtone kama mwenyekiti wa wasanii wa miziki ya injili.

• Amemtaka aendelee kutia juhudi kuipeleka sekta hiyo katika viwango vya juu.

Msanii Janet Otieno amekiri kumtambua Ringtone Apoko kama mwenyekiti wa wasanii wa miziki ya injili nchini Kenya.

Akizungumza na wanablogu, Otieno alisema kwamba Apoko amekuwa akitia juhudi nyingi na hivyo anastahiki kupewa heshima.

Alisema kwamba wanakubali mchango wake katika sekta hiyo na watazidi kushirikiana naye.

"Ringtone, unafanya kazi nzuri na tunakupenda. Endelea kushikilia palepale," Otieno alisema.

Otieno alijitambua kama mwenyekiti mwenza wa Ringtone katika sekta ya miziki ya injili, na kuahidi kushirikiana naye kuipeleka sanaa mbele.

Aidha, alizungumzia suala la Weezdom kudondoka katika misingi ya kikristu na kumtaka msanii huyo kushikilia imani katika Mungu.

Vilevile aliwataka wakenya kudumisha amani kipindi hiki taifa linajiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu.

Hakusita pia kuwaomba mashabiki kuzidi kuwasapoti wasanii ili kuwapa motisha moyo wa kujituma zaidi.