Mcheshi Consumator asema yupo radhi kuwa caretaker ili kupata hela

Muhtasari

• Consumator alisema kwamba yupo tayari kufanya kazi yoyote ili kupata hela za kugharamikia matibabu ya babake.

• Mashabiki walijitokeza kumtakia mzaziwe afueni ya haraka.

Consumator
Consumator
Image: Instagram, KWA HISANI

Mcheshi Peter Wamwea almaarufu Consumator amejitokeza kusema kwamba yupo tayari kuwa caretaker ili kupata hela za kugharamikia matibabu ya babake mzazi.

Consumator alisema kwamba yupo tayari kufanya lolote ili kuhakikisha babake anapona.

"...Chochote ambacho kitanisaidia kupata pesa za kumsaidia babangu anayeugua, nitafanya kwa moyo wangu wote," Consumator alisema.

Alidokeza kwamba amelelewa katika familia ya uwezo wa chini na kukosa hela ni baadhi ya changamoto ambazo anazipitia katika harakati za kuhakikisha wanapata chakula cha kila siku.

Kufikia hatua ya kuomba msaasda kwa umma, inakisiwa kwamba mcheshi huyo alikuwa ametumia pesa zote alizokuwa nazo kwenye matibabu ya babake na maisha kumsukuma ukutani asijue la kufanya.

Mashabiki walijitokeza kutuma pole zao na kumtaka awe na nguvu za kuendelea kuipambania familia yake.

"Kushughulikia familia yako wakati wanapougua kunazua changamoto za kihela, kiakili na kiafya. Naomba Mungu akukutanishe na watu wenye roho nzuri katika kipindi hiki kigumu," shabiki mmoja aliandika.

Kwa muda sasa mashabiki wamekuwa wakitoa maneno makali kwa mastaa wanaoomba msaada kwa umma, wakisema kwamba wanapaswa kuwekeza pesa wanazozipata. 

Hata hivyo mashabiki hao wametakiwa kuwachukulia mastaa hao kama binadamu wa kawaida na kwamba wanaweza kukumbwa na changamoto za kimaisha.