Msanii Ruby asema anatamani kufa, kunani?

Muhtasari

• Ruby amewaacha mashabiki wakikuna vichwa kwa kauli yake ya kutaka kufa.

• Alisema kwamba anataka kupumzika.


Mwanamuziki Ruby amewashangaza mashabiki wake baada ya kupakia ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram akisema kwamba anataka kufa.

Kulingana na ujumbe huo, Ruby alisema kwamba anataka kuondokea mambo mengi na changamoto za dunia.

Mpaka sasa haijajulikana sababu kuu iliyompelekea msanii huyo kuachia kauli hiyo, huku mashabiki na washikadau wakizidi kutoa maoni tofauti.

Wadau pia waliwataka wandani wake kumpigia simu na kumtafuta kuhakikisha yupo salama.

Aidha, baadhi ya watu walikisia kwamba huenda hatua hiyo ilijiri kufuatia mvutano unaoendelea kati yake , Aunty Ezekiel na mpenzi wake wa zamani, Kusah.