Baada ya 'utasa' wa miaka 10, Evelyn Wanjiru apata ujauzito

Muhtasari

• Msanii Evelyn Wanjiru amepata ujazito baada ya subira ya miaka 10.

• Amemshukuru Mungu kwa kumkumbuka, na kuombea wale wote ambao wanahangaika kupata mtoto katika ndoa.

Evelyn Wanjiru na mumewe
Evelyn Wanjiru na mumewe
Image: Instagram, KWA HISANI

Msanii wa muziki wa injili, Evelyn Wanjiru hatimaye amefanikiwa kupata ujauzito baada ya kusubiri kwa miaka kumi.

Wanjiru alisema kwamba Mungu aliyasikia na kuyajibu maombi yake ya muda mrefu.

"Nimekuwa nikingojea msimu huu kwa miaka 10 katika ndoa yangu. Tumbo lililobarikiwa, Mungu ametimiza," Wanjiru aliandika.

Kupitia ujumbe mrefu alioandika katika ukurasa wake wa Instagram, Wanjiru aliwataka wote walio katika ndoa na hawajafanikiwa kupata mtoto kutokata tamaa badala yake kuwa na tumaini kwamba mambo yatakuwa sawa kwa wakati wake.

Hakusita kutoa shukrani kwa mume wake, Agunda Bweni ambaye amekuwa na umuhimu na umuhimu mkubwa katika kipindi hicho cha majaribu na maswali mengi.

Alisema kwamba licha ya changamoto hiyo, waliendelea kumshukuru Mungu na kuamini kwamba Mungu angejibu maombi yao siku moja.

Aidha, aliwashukuru wote ambao waliiombea familia yake walipokuwa wanapitia kipindi hicho kigumu.

Wanamuziki mbalimbali akiwemo Mercy Masika walipelekea katika mitandao ya kijamii kumhongera Wanjiru kwa Mungu kujibu maombi yake ya muda mrefu.