"Hatimaye niko huru!" NaiBoi asherehekea kuvunja mkataba na Universal Music Label

Muhtasari

• NaiBoi - Hatimaye Niko Huru Kutoa Muziki. Hali imekuwa ngumu kwa miaka 3

Msanii NaiBoi
Msanii NaiBoi
Image: Instagram//NaiBoi

Msanii mkongwe kwenye Sanaa ya kizazxi kipya cha Kenya, NaiBoi ni mtu mwenye furaha baada ya kufanikiwa kuutamatisha mkataba wake wa ushirikiano na rekodi lebo ya Universal Music.

NaiBoi ambaye aliingia katika mkataba na lebo hiyo ya kimataifa miaka mitatu iliyopita alieleza kwamba furaha yake imerudi kwa sababu katika kipindi choche cha miaka mitatu amekuwa akishindwa kuachia kazi mpya kwa sababu alikuwa anahisi kama mfungwa.

Miezi michache iliyopita, msanii huyo alielezea wazi kuhusu kutamaushwa kwake kutokana na ambavyo lebo hiyo ilikuwa inaendesha shughuli zake, jambo ambalo siku zote alikuwa anahisi kama linamfunga sana mpaka kushindwa kufikiria utunzi wa kazi mpya.

Staa huyo wa 2 IN 1 alidhihirisha kwamba sasa yuko huru kabisa kuachia kazi zake moto kwa mashabiki wake waliokomaa kwa Subira na Jumanne aliachia kibao chake cha kwanza kabisa tangu kuachiwa huru na Universal Music Label. Kibao kwa jina la Killem Widt au Kamata.

“Imethibitishwa. Hatimaye Niko Huru Kutoa Muziki. Hali imekuwa ngumu kwa miaka 3. Lakini Hey kwa nini Kulalamika wakati naweza Hatimaye Killem widit,” aliandika staa huyo huku akipiga sapoti kibao chake hicho.

Ikumbukwe wanamuziki wengi nchini Kenya wanalilia ngoa nafasi ya kufanya kazi chini ya Lebo hiyo ya Universal Music wakati wengine waliopata nafasi wakitaka kutoka kwa kusema kwamba wanafungiwa kifikira na kimawazo.

Itakumbukwa pia kwamba baada ya kumtambulisha mpenzi wake kama msanii wa kufoka, Bahati aliwahi sema kwamba ataacha kufanya muziki pindi tu mpenzi wake Diana B atapata nafasi ya kuandikishwa mkataba wa kufanya kazi ya muziki chini ya rekodi lebo hiyo.