Size 8, Kambua, Nadia Mukami waongoza wasanii kumpongeza Evelyn Wanjiru kwa ujauzito

Muhtasari

•Size 8 alifurahia ushindi wa Wanjiru kuweza kupata ujauzito hatimaye baada ya kujaribu kwa mwongo mmoja.

•Mtangazaji Massawe Japanni pia hakuchelewa kumpongeza mwanamuziki huyo huku akisema anausherehekea ujauzito wake.

Size 8 na Evelyn Wanjiru
Size 8 na Evelyn Wanjiru
Image: INSTAGRAM// SIZE 8

Hatimaye mwimbaji wa nyimbo za Injili Evelyn Wanjiru ametangaza ujauzito wake wa kwanza baada ya kusubiri miaka 10.

Wanjiru alitangaza habari hizo njema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kusema ujauzito wake ni ahadi ambayo Mungu amemtimizia.

"Leo moyo wangu umejaa furaha na shukrani. Ninapoandika haya, macho yangu yamejaa machozi. Nimekuwa nikingojea msimu huu kwa miaka 10 katika ndoa yangu. Tumbo lililobarikiwa, Mungu ametimiza Ahadi yake katika maisha yetu," Wanjiru alisema.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri wamempongeza msanii huyo kwa kufanikiwa kubeba ujauzito.

Size 8 alifurahia ushindi wa Wanjiru kuweza kupata ujauzito hatimaye baada ya kujaribu kwa mwongo mmoja.

"Alikuja kuniona hospitalini nikiwa mgonjwa sana na siku ambayo nilipewa ruhusa kutoka alikuwa amesimama nami katika maombi. Hatimaye naweza kuchapisha picha hii. Mwangalie Yesu Kristo baada ya miaka 10 ya kusubiri tuna furaha sana wewe," Size 8 alisema kwenye Instagram.

Mtangazaji Massawe Japanni pia hakuchelewa kumpongeza mwanamuziki huyo huku akisema anausherehekea ujauzito wake.

"Moyo wangu umeridhika. Mungu ni mwaminifu," Massawe alisema.

Hizi jumbe za pongezi za baadhi ya wasanii wengine:-

@millywajesus Hongera

@nadiamukami Hongera Wanjiru. Mungu amekukumbuka na naomba awe nawe katika safari hii nzuri. Nakusherehekea.

@mojishortbabaa Hongera watu wangu. Mungu ni mwema

@bettybayo_official Wow! Utukufu kwa Mungu

@joyceomondi Ametenda makuuu