Mimi si shoga, Moya David amjibu Kinuthia baada ya kusema yeye ni mali safi

Muhtasari

• Moya David ametoa tamko kuhusu kauli ya Kinuthia akisema kwamba yeye ni 'mali safi'.

• Hata hivyo alisema kwamba hayo ni mapenzi kutoka kwa mashabiki na anaelewa.

David Moya
Image: Facebook
David Moya
Image: Facebook

Mtumbuizaji katika mtandao wa Tiktok, Moya David hatimaye amemjibu mwenzake katika sekta hiyo kwa kusema kwamba yeye ni 'mali safi'.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Mungai Eve, Moya alisema kwamba kauli hiyo ilikuwa nzuri ila ilitoka kwa mtu asiye sahihi.

"...Ni jambo nzuri lakini sasa imetoka kwa mtu ambaye sio sahihi. Tuache hayo maneno," Moya alisema.

Kauli ya Moya ilijiri baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonyesha Kinuthia akisema kwamba anamtaka Moya David.

"Mtu aniletee Moya, yeye ni mali safi," Kinuthia alisema.

Aidha, Moya alisema kwamba anaelewa  kuwa hiyo ni njia moja ya mashabiki kuonyesha mapenzi kwake, na pia kwa kazi anayoifanya.

"Najua mimi ni mali safi, lakini sasa haikufaa kutoka kwa Kinuthia," Moya David alisema.

Kwa kile kilichoonekana kama njia moja ya Kinuthia kutafuta mbinu ya kufanya kazi naye, Moya alimtaka kufuata mkondo faafu iwapo anataka kumshirikisha katika kazi zake.

Vilevile alisema hakuichukulia vibaya kauli ya  Kinuthia na akadokeza kwamba kuna uwezekano wa kufanya kazi naye.

Ifahamike kwamba Kinuthia kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akificha jinsia yake, jambo ambalo limezidi kuwachanganya mashabiki wake.

Kwa saa mashabiki watalazimika kusubiri kwa muda zaidi kuona iwapo wawili hao wataachia kazi ya pamoja.