"Tangaza mimi ni mke wako, sitaki kufichwa!" Akothee amwambia Nelly Oaks

Muhtasari

• Akothee alimtaka mpenzi wake Nelly Oaks kutangaza wazi kwa umma kwamba yeye ni mke wake halali.

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: Instagram///AKOTHEE

Mwanamuziki Akothee amemtaka mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks kutangaza wazi kwa umma kwamba anamuoa.

Mwanamuziki huyo na mjasiriamali mwenye utata ambaye anajulikana kutomeza maneno yake wakati wa kuwajibu wanaoikanyaga mstari wake wa maisha alimtaka Oaks kutangaza wazi hilo ili lifahamike kwa umma kwa sababu yeye vile alivyo hawezi kufurahia ukosefu wa usalama wa nafsi unaombatana na wasiwasi wa kutojuana iwapo mwenzako anakupenda kweli ama anakuficha masuala kadhaa ndani ya bahari ya huba.

“Hii imeweza na billboard? @nellyyoaks. Lazima atangaze kuwa mimi ni mke wake! Sifurahii wasiwasi na ukosefu wa usalama wa nafsi mimi,” aliandika Akothee kwenye Instagram yake.

Mama huyo wa watoto watano amekuwa katika mahusiano kwa muda na Oaks ambaye alianza kama mratibu na meneja wa shughuli zake za muziki na hivi majuzi Akothee alipokuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa ya miaka 41, Oaks alimsherehekea kwa ujumba maalum wenye mahanjumati yaliyotukuka.

Miezi michache iliyopita, Akothee alitangaza kwamba kabla ya kufika miaka 45, atahitaji kupata watoto wawili zaidi, kabla ya kustaafu kutoka maisha ya umaarufu wa mitandaoni.