"Maisha yangekuwa magumu bila wewe" Kajala Masanja amsherehekea dadake mdogo

Muhtasari

•Kajala ni mmoja wa ambao wamemsherehekea Dorice huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

•Paula amesema anathamini kumbukumbu zake na shangazi huyo wake  na kumshukuru kwa kuwa guzo muhimu katika maisha yake.

Paula Kajala, Kajala Masanja na Dorice Masanja
Paula Kajala, Kajala Masanja na Dorice Masanja
Image: INSTAGRAM// DORICE MASANJA

Dada mdogo wa mwigizaji Fridah Kajala Masanja, Dorice Masanja  anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Familia, marafiki na mamia ya wanamitandao wameendelea kumwandikia kipusa huyo jumbe za kheri njema katika siku hii maalum maishani mwake.

Kajala ni mmoja wa ambao wamemsherehekea Dorice huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake. Kajala amemtambua dadake kama rafiki na mshirika wake mkubwa.

"Hakuna dada bora ambaye ningeweza kuota kuhusu. Wewe ni rafiki yangu mkubwa na mshirika katika uhalifu. Maisha yangekuwa magumu bila wewe. Heri ya siku ya kuzaliwa dada mdogo! Nakupenda sana," Kajala alimwandikia Dorice kupitia Instagram.

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Binti wa pekee wa Kajala, Paula pia alimsherehekea shangazi huyo wake kwa kupakia kumbukumbu yake naye.

Paula amesema anathamini kumbukumbu zake na shangazi huyo wake  na kumshukuru kwa kuwa guzo muhimu katika maisha yake.

"Maisha ya kumbukumbu na wewe ndio hazina bora zaidi ninayoweza kuwa nayo. Asante kwa kuwepo  kila wakati na kunifundisha ukweli mwingi wa maisha haya. Unathaminiwa, nakupenda. HAPPY BIRTHDAY AUNTY," Paula alisema.