Fahamu kwa nini Zuchu aliwahi kataa dili ya 12.5M kuwa balozi wa brand ya pombe

Muhtasari

• African Fact Zone wanaripoti kwamba Zuchu aliwahi kataa dili la milioni 12.5 za kenya kuwa balozi wa kampuni ya kutengeneza pombe.

Msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi
Msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi
Image: Instagram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania, Zuchu ni mmoja kati ya wasanii wasioweka pupa na ulafi mbele ya Imani yake ya kidini.

Inadaiwa kwamba msanii huyo aliyekulia sana katika mazingira ya dini ya Kiislam aliwahi kata dili nono la kuwa balozi wa vileo kwa kusema kwamba dini yake katu haikubali mambo kama hayo.

Kulingana na chapisho moja la African Fact Zone, inadaiwa kwamba kampuni fulani ya vileo iliwahi kumfuata Zuchu huku wakimtaka kumwaga wino ili kuwa balozi wa brand yao hiyo ya vileo kutokana na ufuasi mkubwa wa mashabiki alio nao kwenye mitandao yake ya kijamii.

Dili hiyo ilikadiriwa kuwa ya kiasi cha $108K ambacho ki kiwango sawa na shilingi milioni 12.5 pesa za Kenya lakini akakataa kwa misingi ya Imani ya dini yake.

Baadhi baada ya kupata taarifa hiyo walimsuta Zuchu kwa kukataa dili kubwa kwa misingi ya kidini hali ya kuwa alikubali kuwa balozi wa kampuni na kamari ya Wasafi Bet inayomilikiwa na bosi wake, tena kwa sare kabisa.

Staa huyo wa ‘Sukari’ amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya muziki tangu kujiunga na Wasafi mwaka 2020 na ameandikisha na kuvunja rekodi kadha wa kadha ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mfano, kibao chake cha Sukari ndicho kinachoshikilia rekodi ya kupiga views nyingi zaidi kwa kibao kutoka kwa msanii mmoja ambacho si collabo. Pia Zuchu hivi majuzi aliandikisha rekodi ya kuwa msanii wa kike wa nne katika bara zima la Afrika kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa YouTube, nyuma yqa masataa kama vile Yemi Alade kutoka Nigeria.