'Ulifurahisha shetani,'Ringtone afokea tamasha ya msanii Nyashinski

Muhtasari
  • Ringtone afokea tamasha ya msanii Nyashinski
Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwenyekiti wa Injili Ringtone Apoko hana furaha Jumatatu hii asubuhi na matukio ya iliyomalizika wikendi iliyopita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram msanii huyo mwenye utata wa nyimbo za injili amefokea tamasha ya  Nyashinski iliyofanyika Carnivore.

Kulingana na msanii huyo ambaye pia alikuwa kwenye hafla tofauti siku hiyo hiyo tamasha la real shinski lilikuwa ni shetani pekee ndiye anayefurahi kumwita kwa kuimba kuhusu pombe na wasichana kwa gharama ya neno la kristo.

" DEAR NYANS @realshinski IS BETTER U SINGED FOR WATOTO BADALA YA WALEVI👌💯💪 CARNIVORE ULIFURAHISHA SHETANI NA MAPEPO SHAME AT YOU NYANSNSIKI ⛪," Aliandika Ringtone.

Nyashinski hajamjibu msanii huyo kwa maneno yake, na matamshi yake ya kuudhi.