Wasanii wengi wa Kenya hawajali kuangalia urithi wa muziki-Tedd Josiah

Muhtasari
  • Miaka minane iliyopita, alieleza kwa nini muziki wa Kenya hauna mwendelezo au mguso wa historia ndani yake
  • Kwa mara nyingine Tedd amesisitiza kwa nini muziki wa Nigeria utaongoza kuliko wa Kenya
Tedd Josiah

Mtayarishaji maarufu wa muziki na mbunifu wa mitindo Tedd Josiah amejitokeza kueleza ni kwa nini muziki wa Kenya unaonekana kulegalega.

Miaka minane iliyopita, alieleza kwa nini muziki wa Kenya hauna mwendelezo au mguso wa historia ndani yake.

Kwa mara nyingine Tedd amesisitiza kwa nini muziki wa Nigeria utaongoza kuliko wa Kenya.

"Miaka 8 iliyopita nilisema haya na Wakenya hawakuzingatia….MUZIKI WA NIGERIA UTAWALA!!!! Ndio hapo nimesema na kabla hujaanza kurusha mawe hapa ndio maana nimesema

Hivi sasa Burna boy anaendelea vizuri. KWA NINI? Baba yake alikuwa mshiriki wa bendi ya FELA kutis katika miaka ya 70 Amejifunza kutokana na muziki uliopitishwa kwake Amechukua kutoka urithi wa muziki wa Nigeria na kuchanganya na sauti za kisasa ili kuleta upya. Ana kura milioni 160 Nigeria pekee!

Kenya.... Wasanii wengi hawajali hata kuangalia urithi wa muziki ili kuunganisha kwenye mpya Tuna kura milioni 40 (1/4) ya walichonacho Wanigeria. Wasanii wengi hawaelewi sauti za Kenya za zamani na wanaangalia tu kile wanachosikia sasa, kwa hivyo utafiti wao wa muziki unategemea orodha ya kucheza ya redio za kiss ambayo ni ukweli kwamba nyimbo zote 5 ambazo nyingi ni za Nigeria."