Kuna wale walibet niachane na mume wangu Rommy ila tutagandana mpaka kifo - Shilole

Muhtasari

• Msanii Shilole amesherehekea mwaka mmoja ndani ya ndoa na mume wake, Rommy.

• Amesema kwamba watu ambao walitaka ndoa yao kusambaratika, ila Mungu amewashikilia na kuwaongoza.

Shilole
Image: Instagram

Msanii hatari kutoka Tanzania Zuwena Yusuph Mohammed almaarufu Shilole amesherehekea kwa maneno matamu mwaka mmoja kwenye ndoa na mume wake Rommy.

Kupitia ujumbe mrefu aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Shilole alimshukuru Mungu kwa kushikilia na kuliongoza penzi lao.

Alidokeza kwamba alijuana na Rommy miaka kadhaa iliyopita na hata wakafanikiwa kuwa katika mahusiano ila baadaye wakatengana, huku akionyesha furaha yake kwamba hatimaye waliweza kurudiana.

Kulingana na Shilole, kuna watu wengi ambao walikuwa na dukuduku iwapo ndoa hiyo itadumu, ila kwa hali ilivyo ni wazi kwamba mambo ni mazuri kabisa.

Shilole alikiri kwamba kukutana tena na kufunga ndoa na kipenzi chake ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha, alisema kwamba sifa zote alizozitaka kwa mwanaume anazo Rommy na anashukuru kwa kila wanayojaaliwa kwenye ndoa.

Kuna mashabiki na watu mbalimbali ambao walikuwa wametabiri kwamba ndoa hiyo ingedumu kwa mwezi mmoja tu, ila Mungu ameendelea kutenda makuu katika familia hiyo.

Ifahamike kwamba Shilole amekuwa katika ndoa za awali zenye vurugu kwa mfano ile yake na Uchebe, ila alionekana kuchukulia kila changamoto alizoipitia kama mafunzo ya kumwezesha kufanya zaidi katika ndoa.

Mastaa mbalimbali waliachia kauli zao wakimhongera kwa hatua ambayo wameipiga na kuwatakia miaka mingi pamoja na mpenzi wake.

"...Na iwe kheri mpaka mzeeke aitwe mzee Rommy na wewe bibi Shishi," Ankoo Zumo aliandika.

Kila la kheri kwa wapenzi hawa na kwamba Mungu azidi kuwapa afya na roho ya upendo katika maisha yao.