Nandy arejesha akaunti yake ya Instagram iliyokuwa imedukuliwa

Muhtasari

• Msanii Nandy amesema kwamba amefanikiwa kuirejesha akaunti yake ya Instagram iliyokuwa imedukuliwa.

• Kwa kipindi hicho alikuwa akitumia akaunti ya mumewe.

 

Msanii Nandy

Akaunti ya Instagram ya Msanii Mwimbaji wa Bongofleva Nandy  imerudi baada ya kudukuliwa na watu asiowafahamu siku kadhaa zilizopita.

Nandy alitangaza kupotea kwa akaunti hiyo yenye wafuasi zaidi ya milioni 6.3 kupitia mtandao wa Snapchat baada ya mashabiki zake kutafuta jina la akaunti yake bila mafanikio.

Sasa hivi Instagram ya Nandy imerudi kama ilivyokuwa hapo awali na katika kipindi ambacho akaunti yake ilikuwa hacked alikuwa akitumia akaunti ya mume wake, Billnass.

Hata hivyo hajaweza kuweka wazi kuhusu waliotekeleza kitendo hicho cha kudukua akaunti yake.

Stori za wasanii kudukuliwa akaunti zao za Instagram hazijaanza leo, utakumbuka kwamba mwaka 2015 tatizo kama hilo liliwahi kumkumba msanii Fid Q na Shilole, Linah (2016) na Mkenya Sanaipei Tande (Feb 2021).

 

Msanii Nandy