Diamond - Mwaka huu kuna wasanii wataondoka Wasafi, wawili wapya watatambulishwa

Muhtasari

• Diamond Platnumz alisema kwamba mwaka huu Wasafi inatarajia kuwatambulisha wasanii wengine wawili wapya.

• Pia alisemabaadhi ya wasanii wa sasa katika lebo hiyo wataoneshwa mlango ili kutoa nafasi kwa wengine wapya.

msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz
msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz
Image: YouTube screenshot///BBC Swahili

Staa wa bongo fleva Diamond Platnumz sasa ameweka wazi kuhusu minong’ono inayozidi kukwaruza katika mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya wasanii wamo mbioni kuondoka katika lebo ya Wasafi.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na mtangazaji Salim Kikeke huko BBC L ondon, Dianond aliweka wazi kwamba anafurahia alimtoa Harmonize kimuziki naye Harmonize akawashika mkono wasanii wengine kama Ibraah na Anjella ambao kulingana na Diamond ni kama wajukuu wake kimuziki.

Msanii huyo alisema kwamba kablam waka huu kukamilika lebo yake ya Wasafi inatarajia kuwatambulisha wasanii wengine wawili wapya kwenye kama kama moja ya njia za kuzidi kuinua na kuitanua Sanaa ya Tanzania.

Pia hakusita kugusia kwamba kuna baadhi ya wasanii ambao tayari wamo pale watalazimika kuoneshwa mlango ili kutoa nafasi ya wengine wapya kuingia nao pia kupata nafasi ya kuwashika mkono wasanii wengine kwani sasa washaota mabawa.

“Tunaenda kutambulisha wasanii wengine wawili mwaka huu, na pia mwaka huu si kwamba kila msanii alioko Wasafi atakuwepo. Wengine pia watatoka waanze kujitegemea kufanya shughuli zao,” alisema Diamond.

Platnumz vile vile alisema kwamba atawaunga mkono na kuwapa sapoti ili kuzidi kutamba zaidi nje ya Wasafi na hatowatengenezea mazingira ya chuki.

“Lazima tuwaunge mkono na kuwasapoti, hatuwezi kukuwa na wasanii Wasafi wale wale miaka yote, ni uongo. Hauwezi kusema kwamba leo hii tuko na Mbosso, Zuchu, Rayvanny na Lavalava miaka yote, haiwezekani, lazima na wao waanze kujitegemea,” alisema Simba.

Maneno haya yake yanakuja siku chache tu baada ya uvumi kuzuka kwamba Rayvanny yumo mbioni kuondoka Wasafi huku akijitenga na lebo hiyo kwa kuifuta kwenye utambulisho wa bio yake ya Instagram.