Manzi wa Kibera - Ile Prado TX haikuwa yangu, nilidanganya!

Muhtasari

• “Ile Prado TX haikuwa yangu, ilikuwa ni kupiga misele ya tangazo la kibiashara. Nasema hivi kwa sababu nataka kupanda bodaboda au matatu kwa amani" - Manzi wa Kibera.

Manzi wa Kibera na gari analodai kuwa lake
Manzi wa Kibera na gari analodai kuwa lake
Image: Instagram Screenshot

Mwanamitindo Manzi wa Kibera amewaomba radhi mashabiki wake na kusema kwamba gari aina ya Prado TX aliloonekana nalo kwenye picha abazo alipakia Instagram yake wiki mbili zilizopita si lake.

Wiki mbili zilizopita, mwanadada huyo alizua gumzo mitandaoni baada ya kupakia picha akiwa na gari hilo ambapo kwenye nambari za usajiri palitundikwa jina lake na kufuatisha kwa ‘caption’ kwamba gari hilo ni lake na ndio furaha yake mpya.

Kumbe maskini wa Mungu alikuwa anafukuzia kiki tu kwenye mitandao na baada ya kiki hilo kumuangukia puani ameamua kuweka kila kitu sawa ili kumaliza fikira hizo kwa watu wanaomuona akitumia usafiri wa umma ilhali alisema ako na gari jipya tena nono.

“Ile Prado TX haikuwa yangu, ilikuwa ni kupiga misele ya tangazo la kibiashara. Nasema hivi kwa sababu nataka kupanda bodaboda au matatu kwa amani. Na watu waache kunitazama kwa macho ya kukejeli mitaani. Hilo halikuwa gari langu na siwezi kulimudu, watu wengine watakuwa wamekasirika lakini nimechoka kuigiza na maisha yangu yanazidi kuwa magumu, safari ya 50bob lazima nichukue ubers,” alisema Manzi wa Kibera.