Ni mashoga? Kinuthia adokeza kuchumbiana na Mtumba Man

Muhtasari

• Kinuthia aliandika kwenye Instagram yake dokezo kwamba huenda wanachumbiana na Mtumba Man.

Kinuthia na Mtumba Man
Kinuthia na Mtumba Man
Image: Instagram//Kinuthia

Baada ya muda mrefu wa kukizia kuhusu jinsia yake, hatimaye Kinuthia amefunguka na kuandika kupitia Instagram yake kwamba anachumbiana na Mtumba Man, jamaa ambaye pia anafanya video za TikTok akiwa amevalia nguo za jinsia ya kike kama Kinuthia.

Kwa muda mrefu sasa, watu wamekuwa wakiachwa gizani kuhusiana na jinsia halisi ya mwqanablogu huyo wa TikTok ambaye anajipodoa na kupigina mapambo kama mwanamke huku akidai kwamba yeye ni mwanaume.

Miezi michache iliyopita, Kinuthia katika mahojiano na mkuza maudhui Commentator aliwataka watu waache kujijazia majibu kuhusu jinsia yake kwani yeye mwenyewe hajaiweka wazi.

Lakini sasa ni kama amechoka kificha na hatimaye amefunguka kuhusu maisha yake ya kimapenzi ambapo amewashangaza wengi kwa kusema kwamba anamchumbia Mtumba Man.

“Dawa ya Balloon ni sindano, Mtumba Man utanipenda,” aliandika huku akimalizia na emoji za mapenzi na pete.

Juzi kata waliletana juu na mcheza densi Moya David alipotoa kauli kwamba msakataji huyo ni mali safi, tano ambalo ni maarufu nchini Kenya linalotumika na wanaume wanaoelezea uzuri wa wanawake.

Moya David alimjia juu na kumjibu kwa kumwambia kwamba yeye si shoga na wala hapendi kauli kama hizo kutoka kwa Kinuthia.